BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 5 August 2017

MSUVA ATUPIA MBILI MOROCCO, AONJA USHINDIMchezaji wa zamani wa Yanga, Simon Msuva.

NYOTA wa zamani wa Yanga, Simon Msuva ameendelea kung’ara katika kikosi cha timu yake mpya ya Difaa Hassan El Jadida baada ya juzi Alhamisi kuifungia mabao mawili.

Msuva alifunga mabao hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Club Athletic Youssoufia Berrechid ambao Difaa ilishinda mabao 3-1 na kuwa ushindi wake wa kwanza akiwa na timu yake mpya.


Msuva akifanya yake.

Katika mchezo wa kwanza kirafiki kwa Msuva, Difaa ilifungwa mabao 2-1 ambapo winga huyo alifunga bao hilo pekee kwa timu yake pia alisababisha penalti katika mchezo wa pili wa kirafiki ambao walitoka sare ya bao 1-1.

Akitokea benchi, juzi Msuva aliifungia Difaa mabao mawili na kuiwezesha kupata ushindi huo wa mabao 3-1 huku akionyesha kiwango cha kuvutia kwa timu yake hiyo alipojiunga nayo hivi karibuni akitokea Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jadida, Msuva alivaa jezi namba 77 badala ya ile namba 22 aliyoivaa katika mechi ya kwanza.

Msimu ujao, Msuva anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Difaa katika Ligi Kuu ya Morocco na Ligi ya Mabingwa Afrika.

No comments:

Post a Comment