WEST HAM WACHEZEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 14 August 2017

WEST HAM WACHEZEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI


Romelu Lukaku ndiye mchezaji wa nne Manchester United kufunga mabao mawili mechi yake ya kwanza Ligi ya Premia

Romelu Lukaku alitangaza kuwasili kwake Old Trafford kwa kufunga mabao mawili mechi yake ya kwanza Ligi ya Premia akiwa na Manchester United na kuwasaidia kuwaaibisha West Ham Jumapili.

Timu hiyo ya Jose Mourinho ilitishia West Ham mechi yote na kutoa matumaini kwa mashabiki wa Manchester United kwamba huenda wakawa katika nafasi nzuri ya kufana ligini msimu huu.

Lukaku, aliyenunuliwa £75m kutoka Everton kwa Everton aliwaweka kifua mbele kwa kufunga kutoka kwa pasi ya Marcus Rashford kipindi cha kwanza.

Nyota huyo wa Ubelgiji aliongeza la pili kipindi cha pili kwa kufunga kwa kichwa kutoka kwa frikiki ya Henrikh Mkhitaryan.

Nguvu mpya Anthony Martial aliongeza jingine kabla ya Paul Pogba kukamilisha ushindi huo kwa kombora la mbali.

United sasa wamepoteza mechi moja pekee kati ya mechi 14 za kwanza Ligi ya Premia wakiwa Old Trafford, lakini West Ham nao wameanza msimu kwa kushindwa mara ya 11.

Mourinho alitumia karibu £150m kuimarisha kikosi chake sokoni kwa kumnunua Lukaku kutoka Everton, Nemanja Matic kutoka Chelsea na Victor Lindelof kutoka Benfica.

Ingawa walizidiwa nguvu na Real Madrid katika mechi ya Super Cup ya Uefa, walionekana kuimarika pakubwa Jumapili.