USAIN BOLT:KWAHERI KILA KITU - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 14 August 2017

USAIN BOLT:KWAHERI KILA KITU


https://edusportstz.blogspot.com/

Usain Bolt amesema alikuwa "anasema kwaheri kwa kila kitu" na alikuwa "karibu kulia" alipokuwa
anafikisha kikomo maisha yake kama mwanariadha katika mashindano ya ubingwa wa dunia jijini London.

Bolt, 30, mshindi wa dhahabu mara nane katika Olimpiki, amestaafu kutoka kwenye riadha baada ya kung'aa sana na kujizolea umaarufu si haba.

"Inasikitisha kwamba inanilazimu kuondoka sasa," alisema raia huyo wa Jamaica, ambaye alikimbia kuzunguka uwanja kuwaaga wachezaji uwanja wa michezo wa London Jumapili usiku wa kufungwa kwa mashindano hayo.

"Nilikuwa nasema kwaheri kwa mashabiki na kwaheri kwa mashindano niliyokuwa nashiriki pia."

Alipoulizwa iwapo atarejea kushindana tena, alijibu: "Nimewaona watu wengi sana wakistaafu na kurudi tena halafu hali yao inakuwa mbaya zaidi au wanajiaibisha.

"Sitakuwa mmoja wa watu hao."