SOMA APA UONE KINACHOMTESA ABDI BANDA - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA APA UONE KINACHOMTESA ABDI BANDA




Abdi Banda,

ALIYEKUWA beki wa kati na kiungo wa Simba, Abdi Banda ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Moroka Swallows FC ya nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ amefunguka juu ya kuteswa na ugonjwa wa matatizo ya afya ya akili unaomkabili mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye aliwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu akiwa Sauz, Banda ambaye alidumu kwenye uhusiano na Kabula kwa muda mrefu alisema kuwa, anaumizwa mno na hali iliyompata zilipendwa wake huyo na kibaya zaidi yupo mbali naye, hivyo amekuwa akitumia watu wake wa karibu kumsaidia.
“Nilipokea taarifa za Jini Kabula kwa masikitiko makubwa, japokuwa sijajua chanzo cha tatizo lake ni nini, ninamuombea kwa Mungu apone haraka, nipo mbali ila nawasiliana na watu wangu wa karibu kumsaidia, nimeachana naye miaka miwili iliyopita lakini hawezi kuwa adui yangu, kwani hakuna aijue kesho,” alisema Banda huku Kabula akiwa bado hajapona na tatizo hilo.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz