MTANGAZAJI AHAMISHWA ASITANGAZE MECHI KISA JINA LAKE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Thursday, 24 August 2017

MTANGAZAJI AHAMISHWA ASITANGAZE MECHI KISA JINA LAKE


Mtangazaji wa ESPN ahamishwa kwa sababu ya jina Marekani

Jenerali Robert E Lee na mtangazaji wa ESPN Robert Lee

Shirika la utangazaji la ESPN limemhamisha mtangazaji mmoja kutoka kwenye mechi aliyofaa kutangaza mjini Charlottesville kutokana na jina lake.

Robert Lee amehamishiwa mechi nyingine kwa sababu jina lake linafanana na jina la shujaa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Jenerali Robert E Lee.

Robert Lee alikuwa amepangiwa kutangaza mechi ya Chuo Kikuu cha Virginia dhidi ya Chuo cha William na Mary katika mji huo mnamo tarehe 2 Septemba.

ESPN wamesema wamembadilisha Lee "kwa sababu ya sadfa ya kufanana kwa majina".
Waandamanaji waliokuwa wanatetea ubabe wa wazungu waliandamana katika chuo kikuu hicho mwezi huu.

Maandamano hayo yaliandaliwa kupinga kuondolewa kwa sanamu ya Jenerali Lee, ambaye aliongoza wanajeshi wa majimbo ya kusini yaliyokuwa yanapigania kuendelezwa kwa utumwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani.

Maandamano hayo yalikumbwa na vurugu na mwanamke mmoja aliuawa baada ya gari kuvurumishwa kwenye umati wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga maandamano hayo ya wazungu wababe.

ESPN wametetea uamuzi wao lakini kuna watu ambao wamewakosoa kwenye mitandao ya kijamii.

Bw Lee sasa atatangaza mechi kati ya Chuo cha Jimbo cha Youngstown State na Pittsburgh pia ambayo itachezwa siku hiyo.Sanamu ya Robert E Lee mjini Charlottesville ilikuwa chanzo cha makabili