Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 24.08.201 - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 24.08.201





Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumtaka winga wa Chelsea Willian, 29. (Times)

Chelsea wamepanda dau jipya la pauni milioni 35 kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24. (Telegraph)

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 32 kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27. (Sun)

Nyota wa Chelsea Eden Hazard atafanya kila awezalo kulazimisha uhamisho wake kwenda Real Madrid msimu huu. (Don Balon)

Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk amekutana na Chelsea bila ruhusa ya klabu yake. (Star)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, huenda akaondoka Hispania kabla ya mwisho wa wiki hii. (El Pais)Virgil van Dijk

Kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, anafikiria kutoa taarifa rasmi kwa umma kuzungumzia kutoridhishwa kwake na klabu hiyo, ili kulazimisha uhamisho wake. (Yahoo Sports)

Juventus wanapanga kupambana na Liverpool katika kumsajili beki wa Schalke Benedikt Howedes. (Bild)

Inter Milan wamepanda dau la kumtaka beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, kwa mkopo, katika mkataba wa kumsajili kikamilifu baadaye kwa pauni milioni 20. (Mirror)

Baba yake Lionel Messi amezungumza na Manchester City kuhusiana na mwanae huyo kuhamia Etihad. (Sun)

Kylian Mbappe, 18, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda PSG kwa euro milioni 150. Monaco na PSG tayari zimefikia makubaliano ingawa wanasubiri kuona nani kati ya Julian Draxler, Lucas Moura au Javier Pastore atakuwa tayari kwenda Monaco kama sehemu ya mkataba huo. (L'Equipe)

Beki wa West Brom Jonny Evans, 29, anatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 kwenda Manchester City wiki ijayo. (Mirror)

Manchester City hawajakata tamaa ya kumsajili Alexis Sanchez, 28, na wanafikiria kupanda dau la pauni milioni 50, kumsajili mchezaji huyo kabla dirisha la usajili halijafungwa wiki ijayo. (Times)

Manchester City wanataka kupanda dau la euro milioni 40 kutaka kumsajili beki wa Espanyol Aaron Martin, 20. (Sport)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amezuia uhamisho wa mkopo wa kiungo Andreas Pereira kwenda Valencia. (Marca)

Barcelona wamekuwa na mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusiana na uhamisho wa winga kinda Steven Bergwijn, 19. (gianlucadimarzio.com)

Schalke wamewaambia Barcelona wanaweza kumsajili Leon Goretzka, ili kuzuia mahasimu wao Bayern Munich wasimchukue. (Mundo Deportivo)

Vincent Janssen na Kevin Wimmer wa Tottenham wanakaribia kuhamia West Brom. (Sun)Eliaquim Mangala

Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala anakaribia kuhamia Inter Milan. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain wanafikiria kumsajili kipa wa Napoli Pepe Reina, 34. (AS)

Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa Angel Di Maria, 29, kutoka PSG. (Sport)

Tottenham wanajiandaa kupanda dau jipya kumtaka mshambuliaji wa Lazio Balde Diao, 22, ambaye pia amehusishwa na kwenda Juventus. (Corriere dello Sport)

Liverpool wacharaza Hoffenheim ligi ya mabingwa Uefa

Tottenham wapo kwenye mazungumzo ya kina na PSG kuhusu uhamisho wa beki Serge Aurier kwa pauni milioni 24. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell, 25, ameiambia klabu yake kuwa hataki kwenda popote kwa mkopo msimu huu. (Guardian)

Arsenal watakubali pauni milioni 14 kutoka kwa Deportivo La Coruna ili kumsajili Lucas Perez kabla ya dirisha la usajili kufungwa wiki ijayo. (Evening Standard)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): 


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz