Hizi ndizo Klabu sita za Uingereza kwenye droo Uefa na ratiba zake - EDUSPORTSTZ

Latest

Hizi ndizo Klabu sita za Uingereza kwenye droo Uefa na ratiba zake


Real Madrid walilaza Juventus kwenye fainali msimu uliopita na kuwa klabu ya kwanza kuhifadhi kombe hilo

Klabu sita kutoka Uingereza, tano za England na moja ya Scotland, zinasubiri kwa hamu droo ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambayo itafanyika Alhamisi saa 17:00 BST (saa moja jioni Afrika Mashariki) mjini Monaco.

Mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea, Tottenham waliomaliza wa pili na Manchester City waliomaliza wa tatu wote wamo kwenye droo.

Watajumuika pia na washindi wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Manchester United, pamoja na Liverpool waliofuzu kupitia hatua ya muondoano sawa na mabingwa wa ligi ya Scotland Celtic.

Mechi za hatua ya makundi zitaanza kuchezwa 12-13 Septemba.

Mara ya mwisho wa klabu sita za Uingereza kufika hatua ya makundi ilikuwa mwaka 2007-08 pake klabu za England Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal zilifuzu pamoja na klabu za Scotland Celtic na Rangers.
Liverpool wacharaza Hoffenheim ligi ya mabingwa Uefa

United wakiwa na Sir Alex Ferguson walicharaza Avram Grant na vijana wake wa Chelsea kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti.
Nani wengine wamefuzu?

Mabingwa watetezi Real Madrid wamo kwenye chungu nambari moja pamoja na washindi wengine saba wa ligi kubwa za Ulaya - Chelsea, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Monaco, Spartak Moscow na Shakhtar Donetsk.

Chungu hatari nambari mbili kina klabu za England Manchester United na Manchester City, pamoja na washindi mara tano Barcelona na Paris St-Germain wenye mchezaji ghali zaidi duniani - Neymar.

Klabu za Ligi ya Premia Tottenham na Liverpool zimo kwenye chungu nambari tatu nao Celtic wamo chungu nambari nne ambacho kina pia mabingwa wa Uholanzi Feyenoord na Leipzig waliomaliza nafasi ya pili Bundesliga.

Mechi zitachezwa lini?

Mechi ya kwanza: 12-13 Septemba

Mechi ya pili: 26-27 Septemba

Mechi ya tatu: 17-18 Oktoba

Mechi ya nne: 31 Oktoba-1 Novemba

Mechi ya tano: 21-22 Novemba

Mechi ya sita: 5-6 Desemba
Orodha kamili ya timu

Mada zinazohusiana


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz