SABABU ZA WANAFUNZI KUFELI MTIHANI - EDUSPORTSTZ

Latest

SABABU ZA WANAFUNZI KUFELI MTIHANI




Kwanini wanafunzi wengi wana feli mitihani????Ungana na edusportstz kwa hissani ya Mwl E.D Kinyunyu hili kujua na kufafanua kwa kina sababu na mbinu zitakazo ifanya elimu yetu kupiga hatua. Tembelea kila siku kujuaMakala mbalimbali zinazoandaliwa na Mwl E.D.Kinyunyu kupitia edusportstz



UTANGULIZI:
Wazazi wengi wamekuwa wakipata shida kujua kisababishi cha watoto wao kufeli pindi wamalizapo kidato cha nne. Kwa kiwango kikubwa watu wengi huelekeza lawama zao kwa pande kuu mbili ama upande wawatumishi hasa walimu na upande wapili huelekeza lawama zao kwa serikali kwakuhusisha vikwazo katika upande wa mishahara, makato , na kutotilia mkazo uboreshaji wa mazngira ya walimu hususan nyumba za walimu miundombinu rafiki ya ufundishaji.


KIINI:
Pamoja na lawama hizi ambazo kwakiwango kikubwa zina ukweli naomba pia tujikite kwenye kuangalia kigezo kingine ambacho hiki kitamgusa mwanafuzi moja kwa moja nacho niuchaguzi wamasomo ya kusoma wangali hawajafikia muda mwafaka wakufanya hivyo.


Kwa taratibu za shule zilizo nyingi hapa nchini ni kwamba kwamwanafunzi anayevuka kidato cha pili kwenda channe hutakiwa kuchagua masomo yanayoendana na mchepuo anaotarajia kusoma akiwa advance level yani kidato cha tano na sita. Mfano kwamtu mwenye wazo lakusomea masomo ya sayansi mara nyingi husoma masomo yote yasayansi yani kemia fizikia biolojia na kwabaadhi ya kilimo(agricultural science) na wao huruhusiwa kusoma namasomo ya Sanaa yote WAKATI wale wanaokuwa na ndoto ya kusomea masomo ya Sanaa watakapokuwa advance mara nyingi huwa hawapewi ruhusa kusoma yale masomo ya sayansi.


Kwa utafiti ulofanywa na Mwl E.D.Kinyunyu pamoja na mchunguzi wa blog edusportstz ya umebaini pengo lililopo kati ya wale wanaoruhusiwa kusoma masomo yote na wale wanaosoma masomo machache ambao mara nyingi ni wamasomo saanaa umebaini yafuatatayo;-


  • Wanaokuwa na ndoto Za kusomea masomo ya sayansi hufaulu kwawingi sana ukilinganisha na wanafunzi wamasomo yale machache licha ya wengi kuamin kwamba ukisoma masomo machache unapunguza mzigo wa masomo.

  •  Wanafunzi wanaosoma masomo yote hufaulu kwa ufaulu mkubwa ukilinganisha na wale wa upande wapili.

  • v Miongoni mwa wanaofaulu wengi wao huwa ni wale wanaotarajia kusoma masomo ya sayansi. Lakini pia mara nyingi hufaulu vzuri mbaka masomo ya Sanaa ambayo matarajio ya wengi, huenda wanafunzi wamasomo ya sanaa wangefaulu vizuri Zaidi.


Kutokana na hilo sisi tukiwa miongoni mwa wadau mhimu wa elimu tunapenda kushauri yafuatayo:-


  • Wanafunzi wote wapewe fursa kusoma masomo yote yaani sayansi nayale yasanaa ili kumpa uwanja mpana mwanafunzi kujibu vzuri mitihani yake hasa upande ule au somo litakalokuwa rahisi katika mitihan yake yamwisho. Hii pia inamsaidia mtahiniwa kuwa na masomo ya ziada yatakayohesabiwa ikiwa atayafaulu vzuri ukilinganisha na mengine lakini hayatazingatiwa ikiwa hatoyafaulu ukilinganisha namengine.

  • Wanafunzi kuondoa dhana iliyopo miongoni mwawanafunzi wengi kuwa masomo yasayansi ni magumu kuliko masomo ya sanaaa hii itasaidia kuwekeza nguvu sawa katika masomo yote sayansi na Sanaa.

  • Walimu watumie japo dakika chache ndani ya kipindi au mijadala kuwatia moyo wanafunzi ili kuondosha dhana zisizo na maslahi kwa maendeleo ya kielimu(educational development) badala yake wajikite kuwapa mbinu za namna watakavyoweza kufaulu vzuri mitihani yao hasa ukuzingatia kwamba ujibujibuji namgawanyo wa alama hutofautiano baina ya pande hizi mbili yani sayansi na Sanaa.


  • Wazazi watumie mda mwingi kuwatia moyo wanafunzi namara kwamara washauriane na walimu ili kujua mapungufu mbalimbali yawafunzi ili kwa pamoja kupata njia sahihi ya kuwasaidia wanafunzi hao.


  • Serikali iwezeshe uwepo wa miundombinu rafiki kwa masomo yote hususani masomo ya sayansi ambayo mara nyingi huhitaji vifaa kwa ajili ya masomo kwavitendo (real practicals).

  • Lakini serikali ijikite kuongeza rasilimali watu hasa walimu wa masomo yasayansi pamoja na wataalamu waliobobea katika maswala ya maabara hususani kwashule zilizopo vijijini hasa shule za kata.

  • Na mwisho nawashauri walimu washule hususani wakuu washule kuomba mitihani ya kushindana baina ya shule angalau mbili au tatu mpaka tano kabla ya mitihani ya mock, kanda na taifa ili kuwawezesha wanafunzi kuyazoea maswali na mbinu mbalimbali zakuyajibu maswali ayo, Hii itamfanya mwanafunzi ajiamini pindi anavokuwa kwenye mtihani wa mwisho unaoandaliwa na balaza la mitihani la taifa.

Mwisho:
ufaulu wako pia unategemea jitihada zako binafsi hata kama serikali itawajibika, mzazi na walimu wote wakawajibika kwenye nafasi zao ipasavyo, bado mwanafunzi ana nafasi kubwa sana kuwezesha ufaulu wake kuwa mzuri au mbaya.

KWAMASWALI ZAIDI AU MAONI WASILIANA NASI KUPITIA


· http://Kinyunyuerick1@gmail.com/+255674517224 facebook


· edusportstz@gmail.com/+255757441463


· For edusports facebook


Tembelea kila siku kujua Makala mbalimbali zinazoandaliwa na Mwl E.D.Kinyunyu kupitiaedusportstz


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz