Sidiria yenye uwezo wa kutambua kansa kwa wanawake - EDUSPORTSTZ

Latest

Sidiria yenye uwezo wa kutambua kansa kwa wanawake


Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mexico ameshika headlines duniani baada ya kutengeneza sidiria ‘Brazia’ ambayo ina uwezo wa kugundua saratani ya matiti katika hatua za mwanzo,Teknolojia hii ya kugundua saratani kwa haraka na ufanisi imetajwa kuwa ya kwanza kuwahi kutengenezwa na mtu yoyote duniani.

Julian Rios Cantu, 18, ametajwa kuwa mjasiriamali mgunduzi mdogo zaidi duniani kuwahi kutengeza sidiria ambayo imewekwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kupima hali ya joto na mtiririko wa damu katika matiti, hivyo kuweza kuonesha dalili za ugonjwa wa saratani ya matiti.
Akizungumza na BBC Julian Rios Cantu amesema kuwa alisukumwa kutengeneza siridia hizo ili kuwa msaada kwa wanawake wote duniani baada ya mama yake kugundulika na ugonjwa wa saratani ya matiti. Sidiria hizi zimetabiriwa kupunguza athari zinazoletwa na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa asilimia 70.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz