Ligi Kuu ya NBC iko kwenye hatua za lala salama ambapo mechi nane za mzunguuko wa 29 zitapigwa saa 10 jioni.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa dimba la KMC Complex kuikaribisha TRA United katika mchezo ambao unaweza kuwahakikishia ubingwa mapema kama watashinda na ikitokea wapinzani wao Simba watakosa ushindi dhidi ya Singida BS.
Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopita, matarajio ya Wananchi ni kuona leo wakiibuka na ushindi mwingine kusogea karibu na ubingwa.
Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin amesema wanatarajia upinzani kutoka kwa TRA United lakini anaamini vijana wake watakwenda kupambana kuhakikisha wanachukua alama tatu.
TRA United ni miongoni mwa timu zilizoivurugia hesabu Yanga zilipokutana mkoani Arusha duru ya kwanza mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kumalizika kwa matokeo ya sauluhu ya bila kufungana.
Leo Wananchi hawana mbadala wa matokeo zaidi ya ushindi kwani hata sare inaweza kuwaongezea presha kuelekea mchezo wa mwisho dhidi ya JKT Tanzania siku ya Jumanne.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi hii ya mwisho uwanja wa nyumbani msimu huu.
Usikose kuitazama live kupitia simu yako kupitia app yetu
Bonyeza hapa kudownload App hii utazame sasa
Usikose kutazama mechi zote LIVE kupitia simu yako pia ukiwa na App hii utaweza kutazama mechi zA Caf, mechi zote za ulaya, ligi kuu Tanzania bara, CRDB CUP na nyingine nyingi LIVE kupitia Simu yako
download App hii mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA AU HAPAAAA au HAPAA

Post a Comment