Jioni ya leo Simba Sc itashuka uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es salaam kuikabili Singida BS katika mchezo wa ligi kuu ya NBC raundi ya 29.
Ni miongoni mwa mechi nane za mzunguuko wa 29 ambazo zote zitapigwa muda mmoja, saa 10 jioni.
Vijana wa kocha Steve Barker hawana mbadala wa matokeo zaidi ya ushindi ili kuendelea kusalia kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Barker amesema hawana uwezo wa kuamua matokeo ya mechi nyingine lakini kwa upande wao mpango ni kushinda mechi zote mbili zilizobaki.
Hata hivyo ni wazi wanakwenda kukabiliana na upinzani mkali mbele ya Singida BS ambao wamekuwa na kawaida ya kuipa Simba changamoto kila timu hizo zinapokutana.
Pamoja na kuwa katika misimu miwili iliyopita Simba imeshinda mechi zote za ligi dhidi ya Singida BS, lakini mechi hizo zilikuwa ngumu.
Hata hivyo wakati huu imani ya Wanasimba kushinda mchezo huo ni kubwa zaidi kutokana na ubora wa kikosi chao.
Simba imeshinda mechi nane mfululizo, ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu tangu ujio wa kocha Barker ambaye pia hajapoteza mchezo wowote wa ligi tangu alipojiunga na wekundu hao wa Msimbazi.
Mechi ya leo ni kama fainali kwani ni mchezo ambao pia unaweza kuamua hatma ya Simba kubaki au kuondoa matarajio kwenye mbio za ubingwa.
Usikose kuitazama live kupitia simu yako kupitia app yetu
Bonyeza hapa kudownload App hii utazame sasa
Usikose kutazama mechi zote LIVE kupitia simu yako pia ukiwa na App hii utaweza kutazama mechi zA Caf, mechi zote za ulaya, ligi kuu Tanzania bara, CRDB CUP na nyingine nyingi LIVE kupitia Simu yako
download App hii mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA AU HAPAAAA au HAPAA

Post a Comment