LONDON, ENGLAND: TANGU Ligi Kuu England ianzishwe msimu wa 1992/93, timu 51 tofauti zimecheza kwenye ligi hiyo.
Lakini, ni nani aliyefunga mabao mengi zaidi kwa kila timu? Hapa tunaangalia wafungaji bora wa muda wote Ligi Kuu England kwa kila timu tangu 1992/1993.
Bao la Ollie Watkins kwa Aston Villa dhidi ya Bournemouth Mei 10, 2025 lilimfikisha kwenye mabao 75 ya Ligi Kuu England akiwa na klabu hiyo na hivyo kumpita Gabby Agbonlahor kama mfungaji bora wa muda wote wa Villa katika mashindano hayo.Kwa kuwa Watkins ndiye mchezaji wa hivi karibuni kuwa mfungaji bora wa klabu yake, ni wachezaji gani wengine waliofunga mabao mengi zaidi kwa kila klabu iliyowahi kucheza ligi hiyo?
Harry Kane ndiye mchezaji pekee aliyefunga angalau mabao 200 kwa klabu moja katika mashindano hayo, baada ya nahodha huyo wa England kufunga 213 kwa Tottenham Hotspur kabla ya kuondoka 2023 kwenda Bayern Munich.
Ni timu 10 pekee ambazo zimekuwa na angalau mchezaji mmoja aliyefunga mabao 100 katika ligi hiyo, na wakati huohuo, Alan Shearer ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao 100 au zaidi kwa klabu mbili tofauti katika mashindano hayo, akifunga 148 kwa Newcastle United baada ya awali kufunga 112 akiwa na Blackburn Rovers.
Shearer ni mmoja wa wachezaji wawili pekee wanaoongoza orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu England kwa klabu mbili tofauti, sambamba na Chris Wood.
Mchezaji huyo kutoka New Zealand ana mabao 37 kwa Nottingham Forest, na pia ndiye kinara wa mabao kwa Burnley akiwa amefunga mabao 49 katika ligi hiyo. Lakini, unaikumbuka Cardiff City?
Timu hiyo iliwahi kushiriki Ligi Kuu England na ilikuwa moto kwelikweli na ndiyo yenye mfungaji bora mwenye idadi ndogo zaidi ya mabao katika historia ya michuano hiyo, ambapo Jordon Mutch aliifungia mara saba pekee katika msimu wa 2013 -14.
The post WAFUNGAJI BORA WA KILA TIMU KATIKA EPL appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/1V3zUal
via IFTTT
Post a Comment