Nilivyompata Ndugu Yangu Aliyetoweka Kwa Miezi Minne Baada ya Familia Yetu Kukata Tamaa ya Kumuona Tena

Siku ambayo ndugu yangu alitoweka ni siku ambayo sitawahi kuisahau maishani mwangu. Tulikuwa familia ya karibu sana. Ingawa kila mmoja alikuwa na maisha yake, tulikuwa tunawasiliana mara kwa mara. 

Ndugu yangu alikuwa mtu wa kupenda familia, mchangamfu, na hakuwa mtu wa kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa taarifa.

Ndiyo maana kila kitu kilipoanza, hakuna aliyedhani kingekuwa kikubwa vile. Mwanzoni tuliona kama jambo la kawaida. Kulikuwa na siku simu yake haikupatikana. 

Tulidhani labda alikuwa busy au alisafiri ghafla. Lakini siku zilipoanza kupita bila message wala simu yoyote, moyo wangu ulianza kupata wasiwasi.

Wiki ya kwanza ilipita. Kisha wiki ya pili. Hakukuwa na habari yoyote.Tulianza kuuliza marafiki zake, watu aliokuwa akifanya nao kazi, na hata baadhi ya maeneo aliyokuwa akipenda kwenda. Lakini kila mtu alikuwa anasema kitu kilekile hawakujua alipo.

Polepole hofu ilianza kuingia ndani ya familia yetu. Mama yetu alianza kulia karibu kila siku. Baba alikuwa kimya muda mwingi, lakini ungeona maumivu usoni mwake. Kila simu iliyolia nyumbani tulikuwa tunashtuka tukiamini labda ni habari zake.

Lakini hakuna kilichobadilika. Miezi miwili ilipopita, tulianza kukata tamaa. Watu wengine walikuwa wanatupa stories tofauti tofauti ambazo zilituumiza zaidi. Wengine walituambia tukubali hali ilivyo. Kwa kweli maneno yale yalituumiza sana.SOMA ZAIDI.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post