MSHAMBULIAJI wa Namungo FC, Fabrice Ngoy, ameendelea kuwasha moto katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuongoza orodha ya wafungaji, akiwapiku nyota wa timu za Kariakoo, Yanga na Simba.
Nyota huyo kwa sasa ana mabao nane (8), akionyesha kiwango cha juu na uthabiti mkubwa unaomfanya kuwa gumzo ndani ya ligi hiyo yenye ushindani mkali.
Katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora, Ngoy amewaacha nyuma washambuliaji hatari akiwemo Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depu’, Prince Dube wa Yanga pamoja na Selemani Mwalimu wa Simba, ambao wote wana mabao sita (6).
Uwezo wake wa kufumania nyavu umeifanya Namungo FC kunufaika mara kadhaa, huku mshambuliaji huyo akionekana kuwa tegemeo muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Ngoy alijiunga na Namungo FC akitokea Kitayose FC baada ya kucheza Ligi ya Championship, ambapo alisajiliwa rasmi mwezi Agosti, 2023 na kuanza kuonyesha makali yake mapema.
Kwa kasi aliyonayo sasa, Ngoy anaonekana kuwa tishio kubwa kwa wapinzani wake na mmoja wa wagombea wakuu wa kutwaa kiatu cha ufungaji bora mwishoni mwa msimu huu.
The post NGOY ATAMBA JUU YA YANGA, SIMBA KWENYE MBIO ZA MABAO appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/BcfQEMb
via IFTTT
Post a Comment