MBEGU AIVURUGA MIPANGO YA BOCCO, BARKER AAMUA MAZIMA

KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, ameonekana kumpokonya mamlaka kocha wa timu ya vijana, John Bocco, baada ya kuamua kumbakiza beki wa kikosi cha U-20, Hussein Mbegu, kuendelea kuwa sehemu ya timu kubwa ya Wekundu wa Msimbazi.

Uamuzi huo umechangiwa na kiwango bora alichoonyesha Mbegu katika michuano ya Kombe la Muungano iliyofanyika Zanzibar, ambapo Simba imefanikiwa kutinga fainali na inatarajiwa kukutana na Yanga.

Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kiwango alichoonyesha Mbegu katika mashindano hayo hakiachi nafasi ya kurejeshwa kwenye kikosi cha vijana.

Ameeleza kuwa beki huyo ameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza kwa kujiamini katika eneo la ulinzi, akimiliki mpira vizuri na kuendana na kasi ya soka la kisasa huku akitoa mchango mkubwa kwa timu.

“Kwa kiwango alichoonyesha, naamini hata kocha wa vijana, Bocco, atamwelewa Barker iwapo ataamua kuendelea kumtumia Mbegu katika kikosi cha timu kubwa badala ya kumrudisha kwa vijana,” amesema Ahmed.

Amesema  jukumu la Bocco kwa sasa ni kuendelea kukuza vipaji vingine vitakavyoweza kupandishwa na kuisaidia timu kubwa siku zijazo.

“Bocco anapaswa kuendelea kufanya kazi ya kuibua vipaji vipya kama Mbegu. Tumeona matunda ya juhudi zake, na tunaamini ataendelea kutuletea wachezaji zaidi wa aina hiyo,” ameongeza.

The post MBEGU AIVURUGA MIPANGO YA BOCCO, BARKER AAMUA MAZIMA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/wXZqrgP
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post