MSHAMBULIAJI wa Simba, Selemani Mwalimu, amesema uzoefu alioupata nje ya nchi umemjengea utulivu mkubwa katika mechi za presha, hali inayomsaidia kung’ara kwenye michezo mikubwa bila kuyumba.
Mwalimu ameendelea kuwa mwiba mkali kwa wapinzani wao Yanga, baada ya jana kufunga bao la penalti dakika ya 120 na kuipa Simba ushindi kwenye fainali ya Kombe la Muungano.
Mbali na hilo, mshambuliaji huyo pia aliwahi kufunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ingawa bao lake lilikataliwa na mwamuzi msaidizi, Kassim Mpanga.
Akizungumzia uwezo wake wa kucheza bila presha, Mwalimu alisema siri kubwa ipo kwenye uzoefu alioupata alipokuwa akicheza soka la kulipwa nje ya nchi, hususan katika klabu ya Wydad AC ya Morocco, ambako alipata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa ikiwemo Kombe la Dunia la Klabu.
“Hapa Tanzania hakuna mechi yenye presha kubwa kwangu. Nilishakutana na mazingira magumu zaidi nikiwa nje ya nchi, hasa Wydad AC ambako nilicheza mashindano makubwa. Hii imenisaidia kuondoa kabisa hofu ya mechi kubwa,” amesema Mwalimu.
Kuhusu majukumu aliyonayo ndani ya kikosi cha Simba, ikiwa ni pamoja na kuwa tegemeo la mabao, Mwalimu amesema yuko tayari kubeba jukumu hilo na kupambana kuhakikisha anaiunganisha timu kwa ujumla kuanzia viongozi, benchi la ufundi hadi mashabiki ili kuendeleza mafanikio ya klabu hiyo.
The post KUTOKA WYDAD MPAKA HADI SIMBA, MWALIMU ATOA DARASA LA MECHI KUBWA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/faylNqY
via IFTTT
Post a Comment