CHOBWEDO AFUNGUA VITA YA USAJILI, YANGA WASISITIZA MAPEMA

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea na mzunguko wa pili huku kila timu ikisaka alama tatu muhimu, kiungo mshambuliaji wa TRA United, Ramadhan Chobwedo, ameibuka kuwa kwenye rada za Yanga.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Yanga tayari umeanza kulijadili jina la nyota huyo kwa lengo la kumsajili katika dirisha kubwa la usajili la msimu ujao.

Chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo kimebainisha kuwa kiwango kizuri anachoonyesha Chobwedo ndani ya TRA United kimevutia vigogo hao wa Jangwani, ambao sasa wako tayari kuweka dau mezani ili kuhakikisha wanamnasa.

“Muda wowote kuanzia sasa Yanga wanaweza kumuingiza mchezaji huyo kwenye makubaliano ya awali. Hawataki kusubiri hadi mwisho wa msimu, wameamua kuwahi dili mapema,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, Yanga wanakabiliwa na ushindani kutoka klabu nyingine, ikiwemo Singida Black Stars, ambayo tayari imeshawasilisha ofa kwa mchezaji huyo, huku bado hajafanya uamuzi rasmi.

Kwa upande wake, Chobwedo ameweka wazi kuwa kwa sasa anaendelea kuitumikia TRA United na lengo lake kuu ni kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

The post CHOBWEDO AFUNGUA VITA YA USAJILI, YANGA WASISITIZA MAPEMA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/GE6aY7z
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post