BACCA ATUPA TAULO, AKIRI RUSHINE NI BALAA

KIWANGO kinachooneshwa na beki wa Simba, Rushine De Reuck, kimeendelea kuvuta hisia za mashabiki na wadau wa soka ndani na nje ya uwanja, huku hata wapinzani wakikiri wazi ubora wake.

Safari hii, pongezi hizo zimetolewa na beki wa Yanga, Ibrahim Hamad maarufu kama Bacca, ambaye ameonesha kuvutiwa na namna nyota huyo anavyotekeleza majukumu yake uwanjani.

Bacca amesema tangu kuwasili kwa Rushine ndani ya kikosi cha Simba, safu ya ulinzi imepata mabadiliko makubwa yanayoonekana katika michezo ya hivi karibuni, akibainisha kuwa uwepo wake umeongeza uimara na kuleta hali ya kujiamini kwa wachezaji wenzake.

Amesisitiza kuwa si jambo la kawaida kwa mchezaji kuingia kwenye ligi mpya na kuonesha kiwango cha juu kwa haraka kiasi hicho, hali inayomfanya Rushine kuwa miongoni mwa mabeki wanaoheshimika kwa sasa.

“Naamini Rushine ameongeza kitu kipya kwenye ligi yetu. Ni beki bora sana na wote tumekuwa tukiona kazi yake uwanjani. Anastahili sifa zote kwa sababu anaonesha ubora mkubwa,” amesema Bacca.

Mbali na uwezo wake wa kuzuia mashambulizi, Bacca ameongeza kuwa Rushine anachangia pia katika kujenga mashambulizi kutoka nyuma kwa utulivu mkubwa, jambo linaloifanya Simba kuwa na mfumo imara zaidi wa uchezaji.

Amesema  ushindani uliopo kati ya Simba na Yanga unaendelea kupanda kutokana na uwepo wa wachezaji wa kiwango cha juu kama Rushine, hali inayosaidia kuinua hadhi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ujumla.

The post BACCA ATUPA TAULO, AKIRI RUSHINE NI BALAA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/bHkWIpX
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post