MACHO na masikio ya mashabiki wa soka nchini leo yataelekezwa mkoani Singida, ambako kutakuwa na moja ya michezo ya kusisimua ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Singida Black Stars dhidi ya Simba SC.
Mchezo huo unatarajiwa kuvuta hisia za wengi kutokana na ushindani uliopo kati ya timu hizo mbili.
Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Singida Black Stars katika michezo ya ligi tangu timu hiyo ilipoanza kushiriki Ligi Kuu.
Takwimu zinaonyesha kuwa Simba haijawahi kupoteza mbele ya Singida Black Stars katika michuano hiyo.
Katika michezo nane ya Ligi Kuu iliyozikutanisha timu hizo mbili, Simba imefanikiwa kushinda mara saba huku mchezo mmoja ukimalizika kwa sare. Hadi sasa Singida Black Stars bado haijapata ushindi dhidi ya Simba katika rekodi ya mechi za ligi.
Hata hivyo, licha ya ubora huo katika ligi, Simba bado ina kumbukumbu ya machungu dhidi ya Singida Black Stars baada ya kufungwa mabao 3-1 na kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB msimu uliopita katika hatua ya nusu fainali.
Ushindi huo uliwapa Singida Black Stars kumbukumbu nzuri dhidi ya Simba katika mashindano ya mtoano.
Kutokana na historia hiyo, mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Simba ikisaka kuendeleza ubabe wake katika ligi, wakati Singida Black Stars ikitafuta kuvunja rekodi mbaya na kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Wekundu wa Msimbazi.
The post SIMBA YAINGIA SINGIDA KUENDELEZA REKODI NZURI appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/AHqX9rv
via IFTTT
Post a Comment