SARE waliyoipata Yanga dhidi ya TRA United imezidi kuwapa tahadhari Simba, ambao wanatarajia kushuka dimbani kesho Jumapili kumenyana na wapinzani hao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba watakuwa wenyeji wa TRA United kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, wakilenga kutumia vyema faida ya uwanja wa nyumbani ili kujihakikishia pointi tatu muhimu.
Hii inakuja baada ya Yanga kushindwa kuvuna ushindi mbele ya wapinzani hao, jambo linaloongeza uzito wa mchezo huo.
Katika mchezo uliopita, TRA United walilazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Matokeo hayo yameonekana kuwa onyo kwa Simba, wakihitaji kujiandaa kwa umakini mkubwa ili kuepuka matokeo kama hayo.
Akizungumzia maandalizi ya timu, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi kimewasili na kuingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo muhimu.
Amesisitiza kuwa wanatambua ubora wa TRA United na ugumu wa mchezo unaowasubiri, lakini lengo lao kuu ni kuhakikisha wanapata ushindi.
“TRA United ni mpinzani mgumu sana. Tunaendelea na maandalizi, kikubwa tunahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo wetu huo. Tunatambua haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa mpinzani wetu,” amesema Ahmed .
The post SIMBA WASHTUSHWA NA SARE YA YANGA, WAJIANDAA KIVITA NA TRA UNITED appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/TZLmQJG
via IFTTT
Post a Comment