PIGO BAADA YA PIGO YANGA, JOB AFANYIWA UPASUAJI

KUONGEZEKA kwa majeruhi ndani ya kikosi cha Yanga, kumeendelea kuwa changamoto kubwa kwa timu hiyo katika kipindi hiki cha mashindano, ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hali hiyo imezidi kuwa ngumu baada ya nahodha wa timu hiyo, Dickson Job, kupelekwa nchini South Africa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kufuatia majeraha aliyoyapata.

Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo wa Yanga anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu ili kupatiwa matibabu na muda wa kupona baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

Kutokuwepo kwake ni pigo kwa kikosi hicho ambacho kinapambana kuhakikisha kinaendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Wakati huo huo, hali ya beki mwingine wa timu hiyo, Chadrack Boka, bado haijafahamika vizuri kwani yupo katika vipimo vya kitabibu ili kubaini ukubwa wa jeraha lake. Madaktari wanatarajiwa kutoa majibu rasmi kuhusu hali yake na iwapo ataweza kurejea uwanjani mapema au atalazimika kupumzika kwa muda zaidi.

Akizungumzia hali hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema majeruhi yameendelea kuisumbua timu hiyo licha ya baadhi ya wachezaji kuanza kurejea taratibu kikosini.

Ameeleza kuwa hali hiyo imekuwa changamoto, lakini wanaendelea kupambana kuhakikisha kikosi kinaendelea kuwa imara.

“Jambo la kutia moyo kuwa baadhi ya wachezaji akiwemo Pacome Zouzoua pamoja na Farid Mussa wameanza kurejea kwenye kikosi na hata kuonekana wakikaa benchi katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania FC, jambo linaloashiria kuimarika kwa hali yao ya kiafya,” amesema.

Kamwe ameweka wazi kuwa hali ya mshambuliaji Clement Mzize bado kwani mchezaji huyo hatarajiwi kurejea uwanjani hadi msimu ujao. Hii inaongeza idadi ya wachezaji ambao Yanga inawakosa kutokana na majeraha.

Licha ya changamoto hiyo ya majeruhi, Kamwe amesisitiza kuwa Yanga ni klabu kubwa yenye wachezaji wengi wenye uwezo, usajili uliofanywa pamoja na wachezaji waliopo fiti utaisaidia timu hiyo kuendelea kupambana na kufikia malengo waliyojiwekea katika msimu huu.

The post PIGO BAADA YA PIGO YANGA, JOB AFANYIWA UPASUAJI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/VJEKq5l
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post