KIUNGO wa Yanga, Max Nzengeli, amesema kucheza kwa muda mrefu huku akitumia nguvu nyingi uwanjani ni miongoni mwa sababu zinazoweza kushusha kiwango cha mchezaji kadri msimu unavyoendelea.
Nzengeli ameeleza kuwa ni jambo la kawaida kwa mchezaji anayepata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa dakika nyingi kushindwa kudumisha ubora ule ule kila wakati.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado anaendelea kupambana kwa bidii ili kuhakikisha anaendelea kuisaidia timu yake.
Kungo huyo amesema licha ya changamoto hizo, bado ana ari kubwa ya kufanya kazi kwa juhudi kila anapopewa nafasi ya kuingia uwanjani.
“Nimecheza kwa muda mrefu sana, hivyo ni kawaida kiwango kushuka kidogo ukilinganisha na mwanzo wa msimu. Unapocheza dakika 90 mara kwa mara, lazima mwili uchoke, lakini bado napambana na najitahidi,” amesema Nzengeli.
Ameongeza kuwa hali hiyo haiishii kwenye soka pekee, bali hata katika maisha ya kawaida, mtu anapofanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika vya kutosha, ufanisi unaweza kupungua.
Pamoja na hayo, Nzengeli ameweka wazi kuwa lengo lake ni kurejea katika kiwango chake bora haraka iwezekanavyo ili kuendelea kutoa mchango muhimu ndani ya kikosi cha Yanga kinachoendelea na harakati za mashindano ya ndani.
The post NYOTA WA YANGA AFICHUA SIRI YA KUPOTEZA UBORA WAKE appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/t1EAYKc
via IFTTT
Post a Comment