Katika pilika pilika za ufukwe wa Coco Beach, sauti za wateja na harufu ya vyakula zilipata ladha mpya baada ya Meridianbet kuleta furaha ya kipekee kwa Mama Lishe. Kupitia ugawaji wa aproni, kampuni hiyo iliweka wazi kuwa inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wanawake hawa katika uchumi wa kila siku wa jiji la Dar es Salaam.
Tukio hili lililofanyika Coco Beach, Oyster Bay liliwakutanisha Mama Lishe wengi wanaopambana kila siku kuhakikisha huduma ya chakula inapatikana kwa bei nafuu na kwa ubora. Meridianbet haikuja tu kama mtoa msaada, bali kama mshirika anayeelewa changamoto na ndoto za wajasiriamali hawa wadogo.
Vilevile, Michezo mingi zaidi ya kubashiri inaendelea kupatikana ndani ya Meridianbet ikiwa na ODDS kubwa na machaguo mengi zaidi. Kushiriki ni vyepesi kupitia tovuti ya MERIDIANBET au kwa kupiga *149*10#.
Akizungumza katika tukio hilo, Nancy Ingram kwa upande wa Meridianbet, alieleza kuwa kampuni inaamini katika kuwekeza kwa watu wa chini kabisa wa uchumi ambao ndiyo msingi wa mzunguko wa biashara. Alisisitiza kuwa Mama Lishe sio tu wateja wao, bali ni sehemu ya familia kubwa ya Meridianbet, hivyo wanastahili kupewa sapoti ya kweli na endelevu.
Furaha na shukrani zilitawala mioyo ya kina mama hao, wakieleza kuwa msaada huo ni chachu ya kujiamini zaidi na kuboresha muonekano wa biashara zao. Kwao, ilikuwa ni ishara kuwa juhudi zao zinaonekana na zinathaminiwa na taasisi kubwa kama Meridianbet.
Kwa hatua hii, Meridianbet inaendelea kujenga daraja kati ya burudani na maisha halisi ya jamii. Inaonyesha wazi kuwa ushindi sio tu kwenye michezo ya kubashiri, bali pia katika kugusa maisha ya watu, kuwawezesha na kuwapa matumaini mapya ya kesho iliyo bora zaidi.
The post MERIDIANBET YAWAINUA MAMA LISHE KWA VITENDO COCO BEACH appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/3asDTCt
via IFTTT
Post a Comment