MABORESHO YA JANUARI SIMBA SAFARI YA UBORA, MAGORI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, amesema kuwa kutokana na maboresho yaliyofanywa Januari katika dirisha dogo la usajili, timu hiyo inatarajiwa kuonyesha kiwango bora zaidi katika siku zijazo.

Amesema kitendo cha kuondoka kwa wachezaji saba kati ya kikosi cha kwanza na kuingia kwa wachezaji saba wapya si jambo dogo, bali ni hatua kubwa inayopaswa kupongezwa kwani inaonyesha mpango wa kimkakati wa kuimarisha timu.

Magori pia ametoa wito kwa mashabiki wa Simba kuacha fitina na ugomvi, akisisitiza kuwa umoja ndio silaha kubwa zaidi katika kurejesha timu katika kiwango chake cha juu. Amesema mshikamano wa kila Mwanasimba ni muhimu katika safari ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Ameeleza kuwa mechi za Simba zimekuwa ngumu kutokana na ushindani mkali, lakini changamoto hizo ni sehemu ya mpira halali na wa ushindani. Mashabiki wanapaswa kuwa na imani na mwelekeo wa timu, kwani kila mchezo unalenga kupata matokeo chanya.

“Lengo letu ni kuendelea kucheza kwa juhudi na nidhamu ile ile tuliyojiwekea tangu mwanzo wa msimu. Simba haitayumba kwa maneno ya pembeni bali itaendelea kupambana uwanjani kuhakikisha inapata matokeo chanya,” amesema Magori.

Aameeleza kuwa timu inazidi kuimarika siku hadi siku. Mabadiliko makubwa ya Januari, ambapo wachezaji saba waliokuwa kikosini walitolewa na wachezaji saba wapya kuingizwa, yameanza kuonyesha matokeo chanya huku wachezaji wakizoeana katika mfumo wa timu.

Magori anaamini kuwa kwa mshikamano wa timu na sapoti ya dhati kutoka kwa mashabiki, Simba inaweza kurejea katika kiwango chake bora, kufikia malengo yake, na kutwaa taji kama ilivyokusudiwa msimu huu.

The post MABORESHO YA JANUARI SIMBA SAFARI YA UBORA, MAGORI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/zoOPrnq
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post