LIGI NI MARATHON, MT KUPIGA HATUA MECHI ZIJAZO, PEDRO

BAADA ya kuvuna alama moja mbele ya Azam FC, Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club, Pedro Goncalves, ameanza kutangaza vita ya kusaka pointi tatu kwa wapinzani wao katika michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ilishindwa kuonyesha makali yake jana baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Azam FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Goncalves amesema ulikuwa ni mchezo mgumu na wa ushindani mkubwa kutokana na ubora wa mpinzani waliyekutana naye, jambo lililofanya timu zote kushindwa kupata mabao licha ya jitihada walizozionyesha uwanjani.

Kocha huyo alikiri kuwa alama moja waliyoipata haikuwa malengo yao makuu, lakini akaeleza kuwa si matokeo mabaya sana kwa kuwa ligi ni ndefu kama mbio za marathon, hivyo bado wana nafasi ya kurekebisha makosa na kufanya vizuri katika michezokurekebisha

Amesisitiza kuwa kikosi chake kitaendelea kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha kinapata ushindi katika mechi zijazo, hasa zile za ugenini ambazo zimebaki katika ratiba ya ligi.

“Vijana wamepambana kutafuta pointi tatu lakini hatukufanikiwa. Sasa tunajiandaa na mchezo ujao wa ugenini, ambapo tunalenga kupata alama sita katika mechi mbili zijazo,” amesema Goncalves.

The post LIGI NI MARATHON, MT KUPIGA HATUA MECHI ZIJAZO, PEDRO appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/THxXAG1
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post