Golden Matrix Group imetangaza rasmi kubadilisha jina lake na sasa itatambulika kama Meridian Holdings Inc. Kuanzia tarehe 3 Machi 2026, kampuni hiyo itafanya biashara kwenye Nasdaq Capital Market kwa alama mpya ya MRDN. Mabadiliko haya yanaakisi ukuaji wa haraka na upanuzi wa shughuli zake katika masoko ya kimataifa. Ni hatua inayolenga kuimarisha taswira ya kampuni mbele ya wawekezaji na washirika wa kibiashara duniani.
Kubadilishwa kwa jina kunalenga kuoanisha utambulisho wa kampuni na chapa yake kuu ya Meridianbet, ambayo imekuwa nguzo ya mafanikio yake kimataifa. Kwa sasa, Meridian Holdings inasimamia taasisi sita muhimu ambazo ni Meridianbet, Expanse Studios, RKings, Classics for a Cause, GMAG na Mexplay. Muundo huu unaonyesha upana wa uwekezaji wake katika michezo ya kubashiri, teknolojia na burudani.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Hatua hii imekuja muda mfupi baada ya kukamilika kwa ununuzi wa Fairbet Ltd. nchini Malta, ambapo Meridianbet imechukua umiliki wa asilimia 100 wa shughuli zake. Kupitia ununuzi huo, mtandao wa maduka ya rejareja umeongezeka kwa vituo tisa na kufikia jumla ya 20. Sasa kampuni inaendesha zaidi ya mashine 60 za kubashiri michezo na mashine 120 za sloti katika maeneo ya Malta na Gozo.
Sambamba na mageuzi hayo, Meridian Holdings Inc. imetangaza mpango wa kuunganisha hisa ili kuboresha muundo wake na kuongeza mvuto kwa wawekezaji wa taasisi. Mkakati huu unalenga kuoanisha thamani ya hisa na viwango vya kimataifa vya sekta ya michezo ya kubahatisha.
Afisa Mtendaji Mkuu, Zoran Milosevic, amesema mabadiliko ya kuwa Meridian Holdings yanaakisi hali halisi ya biashara ya kampuni leo. Amesisitiza kuwa kwa Meridianbet kuwa chapa kinara na kwa kuzingatia mafanikio ya upanuzi nchini Malta, kampuni imeamua kuunganisha utambulisho wake ili kuwahudumia vyema zaidi wanahisa wake na masoko yote inayofanyia kazi.
The post GOLDEN MATRIX GROUP YAANZA SAFARI MPYA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/2kGQEOZ
via IFTTT
Post a Comment