CAMARA AWEKA MSIMAMO MKALI NDANI YA SIMBA

KIPA wa klabu ya Simba SC, Moussa Camara, ameonyesha dhamira kubwa ya kupambana baada ya kutuma ujumbe mfupi lakini wenye uzito kupitia mitandao yake ya kijamii akisisitiza kuwa hana muda wa kupoteza katika harakati za kusaka mafanikio.

Ujumbe wake aliouandika katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ukisema, “Hiyo tayari inatosha, hakuna muda wa kupoteza,”

Umetafsiriwa na mashabiki wengi kama ishara ya kujiamini na ari mpya ya kupambana. Kauli hiyo inaonyesha wazi kuwa kipa huyo ameweka nguvu zake katika kurejea kwenye ubora wake ili aweze kuisaidia timu yake.

Kwa sasa Camara amekuwa nje ya kikosi kwa muda kutokana na majeraha yaliyomsumbua, lakini anaendelea na programu maalum ya mazoezi chini ya uangalizi wa madaktari wa timu ili kurejesha utimamu wake wa mwili kwa asilimia 100.

Hatua hiyo inaonyesha dhamira yake ya kutaka kurejea uwanjani haraka iwezekanavyo na kuendelea kutoa mchango kwa timu hiyo yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.

Kipa huyo raia wa Guinea amekuwa miongoni mwa nyota muhimu ndani ya kikosi cha Simba, akitoa mchango mkubwa langoni kwa kuokoa hatari katika michezo mbalimbali na kusaidia timu hiyo kubaki kwenye ushindani mkali wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mashabiki wa Simba wana matumaini kuwa kurejea kwake kutaimarisha zaidi safu ya ulinzi ya timu hiyo na kuongeza nguvu katika harakati za kusaka ushindi katika michezo ijayo ya ligi.

The post CAMARA AWEKA MSIMAMO MKALI NDANI YA SIMBA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/NS4b67l
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post