Binti aomba talaka wiki moja baada ya harusi kugundua mume ana wake wawili TikTok

Ilikuwa ni harusi iliyovutia wengi, picha zilizosheheni mitandao, mavazi ya kifahari, muziki wa moja kwa moja na wageni waliomiminika kushuhudia kiapo cha mapenzi. 

Lakini siku saba tu baada ya sherehe hiyo, binti mmoja mwenye umri wa miaka 24 alijikuta katika ofisi ya wakili akiwasilisha ombi la talaka baada ya kugundua kuwa mume wake alikuwa tayari na wake wawili wengine aliokuwa akiwaficha kupitia akaunti za siri za TikTok.

Kisa hicho kilichotikisa familia mbili kimetokea katika kaunti ya Kiambu, ambapo wanandoa hao walikuwa wameanza maisha yao mapya kwa matumaini makubwa. 

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na familia ya binti huyo, hakukuwa na dalili zozote za tatizo kabla ya harusi. Uchumba wao ulienda haraka, maandalizi yakafanyika ndani ya miezi sita, na kila kitu kilionekana sawa.

Lakini ukweli ulianza kujitokeza kwa njia isiyotarajiwa.Soma Zaidi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post