BARKER AFICHUA SIRI YA MPANZU, DAKIKA ZA MWISHO

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steven Barker, ameweka wazi siri ya maelekezo aliyompa kiungo wake Elie Mpanzu kabla ya kuingia uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars.

Barker amesema kabla ya kumuingiza Mpanzu alimweleza wazi umuhimu wa kucheza kwa utulivu katikati ya uwanja na kuhakikisha anaisaidia timu kudhibiti mpira ili kupunguza presha kutoka kwa wapinzani.

Amesema maelekezo hayo yalikuwa sehemu ya mpango wa kuhakikisha Simba inapata matokeo mazuri katika uwanja wa ugenini.

Kwa mujibu wa kocha huyo, Mpanzu alionesha nidhamu kubwa ya kiuchezaji mara baada ya kuingia uwanjani, akitekeleza majukumu yake ipasavyo na kusaidia timu kupata uwiano mzuri wa mchezo kuanzia safu ya kiungo hadi ushambuliaji.

Barker ameeleza  kuwa uwezo wa kiungo huyo kusoma mchezo na kucheza kwa utulivu uliipa Simba nafasi ya kumiliki mpira zaidi na kuanza kutengeneza nafasi za kushambulia, jambo lililobadili mwelekeo wa mchezo huo uliokuwa mgumu.

Kocha huyo pia amesisitiza kuwa nidhamu ya kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ni jambo muhimu kwa wachezaji wake, akisema mara nyingi ushindi hutegemea namna ambavyo wachezaji wanatekeleza mbinu walizopewa.

“Niliwaambia wachezaji wangu kwamba mechi huchezwa hadi dakika ya 95 au 96, hivyo ni lazima kupambana hadi mwisho. Ni vizuri kuona Mpanzu aliingia na kufunga bao la ushindi,” alisema Barker.

Ameongeza  kuwa haikuwa kazi rahisi kwa Simba kupata ushindi dhidi ya Singida Black Stars, kwani walilazimika kupambana kwa nguvu hadi dakika za mwisho ili kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu.

Barker amesema  kuwa katika soka ushindi unaweza kupatikana wakati wowote, hata katika dakika za mwisho, akiwapongeza wachezaji wake kwa kuonesha moyo wa kupambana na kuamini hadi walipopata bao la ushindi.

The post BARKER AFICHUA SIRI YA MPANZU, DAKIKA ZA MWISHO appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/sHGvR3p
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post