MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Sports Club, Ahmed Ally, ameonekana kutupa kijembe kwa watani wao wa jadi Yqnga baada ya kueleza kuwa hawana presha yoyote juu ya nafasi ya kileleni katika Ligi Kuu Tanzania Bara, akisisitiza kuwa muda ukifika watawashusha.
Ahmed amesema kauli yake inaashiria kuwa Simba hawashtushwi na Yanga kuongoza ligi kwa sasa, kwani anaamini mambo yanaweza kubadilika kadri msimu unavyoendelea.
Ameeleza kuwa katika soka lolote linawezekana na timu yao ina uwezo wa kurejea juu ya msimamo wakati wowote.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Simba wanaamini kuwa siku ikifika watakutana na wapinzani wao hao na kufanikisha lengo lao la kuwashusha kutoka nafasi ya juu.
Ameongeza kuwa wanachohitaji kwa sasa ni kuendelea kujipanga vizuri na kuhakikisha wanapata matokeo chanya katika kila mchezo uliopo mbele yao.
Amesema kuwa moja ya michezo muhimu inayosubiriwa na mashabiki ni ule wa duru ya pili wa Kariakoo Derby kati ya Simba na Yanga, ambao unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium. Katika mchezo huo, Simba watakuwa wenyeji wakiamini wataweza kupata ushindi.
Ahmed ameeleza kuwa kucheza nyumbani kunawapa motisha kubwa wachezaji pamoja na mashabiki wao, hivyo anaamini timu yao itaingia uwanjani ikiwa na morali ya juu ya kupambana na kuibuka na alama tatu muhimu.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa kwa sasa benchi la ufundi na wachezaji hawajielekezi zaidi kwenye derby hiyo, bali wanaangalia michezo ya karibu ambayo ni muhimu katika kukusanya alama.
Amesema malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanapata ushindi katika kila mechi iliyopo mbele yao ili kuendelea kusalia kwenye ushindani wa ubingwa wa ligi msimu huu.
Wakati huo huo, Ahmed amesema kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Pamba Jiji FC.
Simba wanatarajiwa kushuka dimbani Alhamisi, Machi 19, ugenini katika Uwanja wa CCM Kirumba Stadium wakilenga kuondoka na pointi tatu muhimu.
The post AHMED AICHIMBA YANGA, UONGOZI WAO WA MDA TU appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/jr32aVn
via IFTTT
Post a Comment