UONGOZI wa klabu ya Yanga umekuri kuwa kila inapokutana na Namungo FC, hasa ugenini, huwa inakumbana na upinzani mkali na wakati mwingine kupata wakati mgumu wa kusaka matokeo.
Kikosi cha Yanga kimeondoka leo Ijumaa, Februari 21, 2026 majira ya saa tatu asubuhi kuelekea Ruangwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji wao, Namungo FC
Mabingwa hao wa kihistoria wameamua kusafiri siku moja kabla ya mchezo huo muhimu ili kuwapa wachezaji muda wa kutosha kupumzika na kuzoea mazingira ya Ruangwa.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili, Februari 22, 2026 majira ya saa moja kamili usiku katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, mkoani Lindi. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wake katika mbio za ubingwa msimu huu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, wamejiandaa kwa tahadhari wakitambua ubora na ushindani wa wapinzani wao wanapokutana nao katika uwanja wao wa nyumbani.
“Namungo FC wanaweza kutugea maajabu. Mara nyingi wamekuwa wakitusumbua sana tunapokutana nyumbani kwao. Tunapata shida tunapocheza nao, hivyo tunahitaji umakini mkubwa,” amesema Kamwe.
Yanga wanahitaji matokeo chanya ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi, Namungo nao wakisaka alama muhimu mbele ya mashabiki wao wa nyumbani katika pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa.
The post YANGA YATAMBA, UBABE WA NAMUNGO MAJALIWA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/PALQWZ4
via IFTTT
Post a Comment