PEDRO KILA KITU REHANI, YANGA KUPIGANIA ROBO FAINALI

KOCHA wa Yanga, Pedro Goncalves, ameweka wazi kuwa kikosi chake hakina jambo jingine kichwani kwa sasa zaidi ya kushinda na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa kocha huyo, malengo ni moja tu Jumapili hii  kuibuka na ushindi dhidi ya JS Kabylie na kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Yanga watakuwa wenyeji katika mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi utakaopigwa Jumapili,  Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.

Faida ya kucheza nyumbani inatajwa kuwa moja ya silaha muhimu kwa Wananchi, huku wakitarajia sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao watakaofurika kuishangilia timu yao.

Hata hivyo, hesabu za kufuzu bado zinaonekana kuwa ngumu. Matokeo ya mchezo mwingine kati ya Al Ahly na FAR Rabat yanaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika hatima ya Yanga.

Endapo FAR Rabat itapata ushindi, hali hiyo inaweza kuifanya Yanga kuwa katika wakati mgumu zaidi wa kusonga mbele, jambo linalowalazimu kupambana kwa nguvu zote bila kutegemea msaada wa matokeo ya pembeni.

Wakati mashabiki wakihangaika kupiga mahesabu na kuombea matokeo mazuri kutoka katika mchezo wa Al Ahly dhidi ya FAR Rabat, benchi la ufundi la Yanga limeamua kuhamishia nguvu zote uwanjani.

Pedro amesisitiza kuwa timu yake haitakiwi kuyumba kisaikolojia kwa kuangalia kinachoendelea kwingine, bali ijikite katika kutimiza wajibu wake wa kushinda.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya kambi ya Yanga, maandalizi yamekuwa makini na yenye umakini mkubwa, huku wachezaji wakionyesha ari na morali ya hali ya juu.

Pedro ameandaa mkakati maalum wa kiufundi na kisaikolojia ili kuhakikisha kikosi chake kinacheza kwa nidhamu, umakini na ufanisi mkubwa mbele ya lango.

Sasa macho na masikio ya Wananchi yote yataelekezwa New Amaan Complex, wakiamini kuwa chini ya Pedro, Yanga inaweza kuandika historia nyingine kwa kutinga robo fainali.

Kila kitu kitaamuliwa ndani ya dakika 90, ambapo ushindi pekee ndio tiketi ya ndoto za kuendelea na safari ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post PEDRO KILA KITU REHANI, YANGA KUPIGANIA ROBO FAINALI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/0I9EUgj
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post