Niliishi Kwa Hofu Kwa Sababu Kila Niliyempenda Alipata Msiba Ndani ya Mwaka

Nilianza kuamini kuwa mimi si wa kawaida. Haikuwa kwa sababu nilikuwa na tabia mbaya au historia ya ajabu, bali kwa sababu kila mwanaume niliyemruhusu aingie moyoni mwangu alikumbwa na msiba mkubwa ndani ya mwaka mmoja.

Wengine walipoteza wazazi, wengine walipata ajali mbaya, na mmoja alipoteza kazi na kuanguka kwenye msongo wa mawazo uliomfanya anikimbie kabisa.

Mara ya kwanza nilidhani ni bahati mbaya tu. Tulikutana chuoni, tukapendana kwa dhati. Miezi nane baadaye baba yake alifariki ghafla. Alibadilika kabisa. Alianza kuniona kama mzigo wa ziada katika maisha yake yenye huzuni. Hatukudumu.

Nilipokutana na wa pili, nilikuwa tayari nimepona maumivu ya kwanza. Nilimpenda kwa tahadhari.

Lakini ndani ya miezi kumi, mama yake aliugua na kufariki. Nilikuwa pembeni nikimfariji, lakini familia yake ilianza kunitazama kwa jicho la mashaka. Waliniona kama kivuli kibaya kilichoingia na kuondoka na furaha yao. Ndoa haikuwahi kutajwa tena.

Nilijaribu kujipa muda. Nilihama mji, nikaanza kazi mpya. Hapo ndipo nilikutana na mwanaume wa tatu. Alikuwa mchangamfu, mwenye mipango, na alinitambulisha kwa ndugu zake mapema. 

Nilianza kuamini labda mkosi umeisha. Lakini kabla hatujafikisha miezi kumi na miwili, kaka yake alipata ajali mbaya ya barabarani. 

Msiba ule ulivuruga familia yao. Pole pole alianza kuniweka mbali, kana kwamba uwepo wangu ulimkumbusha maumivu.Soma Zaidi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post