WACHEZAJI wanaocheza timu za Ligi Kuu Bara, wameanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), baada ya kufunga ‘Hat-Trick’ mbili kabla ya mechi za jana, ikiwa ni idadi kubwa kwa nyota hao tofauti na msimu uliopita wa 2024-2025, waliofunga moja.
Msimu huu wa 2025-2026, ‘Hat-Trick’ tatu zimefungwa ikiwa ni hatua ya 64 bora ya michuano hiyo na mbili ni za nyota wa Ligi Kuu, ambao ni Yassin Mgaza wa Dodoma Jiji aliyeifungia timu hiyo kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kilimanjaro Wonders.
Nyota mwingine anayecheza Ligi Kuu aliyefunga ‘Hat-Trick’ ni Paul Peter wa JKT Tanzania na mshambuliaji huyo alifunga mabao manne, wakati kikosi hicho kiliposhinda mabao 7-0 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 1982, Pan Africans.
Katika ‘Hat-Trick’ hizo tatu, nyingine imefungwa na mshambuliaji wa Transit Camp, Omary Ramadhan, wakati kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Championship kiliposhinda mabao 4-0 dhidi ya Chama la Wana ya Njombe.
Msimu uliopita wa michuano hiyo, ‘Hat-Trick’ nne zilifungwa huku wachezaji wa Ligi ya Championship wakitawala zaidi kwa kufunga tatu kati ya hizo, huku moja pekee ikifungwa na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI raia wa Burkina Faso.
Katika msimu wa 2024-2025, Aziz KI anayeichezea kwa sasa Al-Ittihad SC ya Libya, aliifungia Yanga ‘Hat-Trick’ wakati kikosi hicho kikiifunga Stand United ‘Chama la Wana’, mabao 8-1 kwenye mechi ya hatua ya robo fainali, Aprili 15, 2025.
Nyota watatu waliofunga ‘Hat-Trick’ msimu huo wanaocheza Ligi ya Championship, walikuwa ni Kassim Shaibu ‘Mayele’ anayeichezea kwa sasa Mtibwa Sugar, ambapo aliifungia TMA ya Arusha, wakati kikosi hicho kikishinda mabao 5-1 dhidi ya Leopards FC, Desemba 5, 2024.
Elias Maguri anayeichezea Dodoma Jiji kwa sasa, aliingia pia katika kumbukumbu za nyota waliofunga ‘Hat-Trick’ na nyota huyo aliifungia Biashara United kwenye ushindi wa kikosi hicho wa mabao 5-0 dhidi ya TRA FC, Desemba 7, 2024.
Mfungaji bora wa Ligi ya Championship msimu wa 2024-2025, Raizin Hafidh aliyefunga mabao 18, akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar anayocheza hadi sasa, aliifungia ‘Hat-Trick’ katika michuano hii, wakati wa ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Town Stars, Machi 3, 2025.
Kabla ya mechi za jana, tayari wachezaji wawili wa Ligi Kuu Bara wameshafunga ‘Hat-Trick’ katika Kombe la FA msimu huu, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tofauti na msimu uliopita, huku nyota wanaocheza Ligi ya Championship wakianza pia vizuri, jambo linalosubiriwa kuona mwishoni itakuwaje.
MATOKEO HATUA YA 64 BORA
Transit Camp 4-0 Chama la Wana
Coastal Union 3-1 Nyumbu
Fountain Gate 1-0 Mapinduzi
KMC 3-3 Bandari Tanzania (penalti 2-3)
Dodoma Jiji 3-1 Kilimanjaro Wonders
Simba 3-0 Greenland
Mbeya Kwanza 5-0 FGA Talents
Kagera Sugar 5-0 Mighty Elephant
Geita Gold 1-0 Kajuna
B19 7-0 Dhujau
Barberian 1-1 Kijiweni Nongwa (penalti 2-4)
Songea United 2-1 Vijana
Bigman 0-1 Nyika
Yanga 2-0 Cosmopolitan
Hausang 2-1 West Sengers
Stand United 4-0 Mabao
African Sports 4-1 Kilimo
JKT Tanzania 7-0 Pan African
Mtibwa Sugar 5-0 IAA SC
Pamba Jiji 1-1 Alliance (penalti 4-2)
Mashujaa 1-0 Nkim
The post MASTAA LIGI KUU WAJIBU MAPIGO FA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/TJMx1SG
via IFTTT
Post a Comment