JKT TANZANIA YAKARIBIA MALENGO YA MSIMU

KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema wanayasogelea malengo yao ya msimu huu, aliyoyataja ni ubora wa timu kila inapocheza mechi, wachezaji viwango vyao kuwa juu na kuhakikisha wanamaliza nafasi nzuri zaidi katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Msimu uliopita, JKT Tanzania ilimaliza nafasi ya sita, katika mechi 30 ilishinda nane, sare 12, ikapoteza 10, ilifunga mabao 27 na kuruhusu mabao 27 huku ikivuna pointi 36.

Jambo ambalo kocha huyo amesema wana deni la kuhakikisha wanamaliza ligi siyo chini ya nafasi ya sita, ikiwezekana wapande juu zaidi, hilo ndilo wanalolipambania zaidi.Ligi inayoendelea JKT Tz imecheza mechi 16, imeshinda saba, sare saba, imepoteza mbili, inamiliki mabao 18, imetikiswa nyavu zake mara 10, ina pointi 28 kileleni mwa msimamo.

“Japokuwa ligi ni ngumu ila hatuna budi kuyapambania malengo hadi yatimie,” amesema kocha huyo.

Aliongeza: “Ugumu wa msimu huu unatokana na viongozi wa klabu wanavyoziandaa timu zao vizuri, mbinu za makocha na wachezaji wenyewe wana ushindani mkali, hivyo siyo rahisi mechi kumalizika na kutoka na pointi tatu iwe nyumbani ama ugenini.”

Ukiachana na hilo, alimzungumzia beki wa Simba, Wilson Nangu anayeuguza majeraha kwamba anapaswa kukubaliana na hali, kisha aamini atapona na maisha mengine yataendelea.

“Kazi ya mpira wa miguu inatumia nguvu na mwili, hivyo kupata injari ni ajali kazini pia azingatie kile anachoelekezwa na daktari, vivyo hivyo kwa Yakoub Suleiman aliumia tukiwa Morocco na timu ya Taifa, nilimwambia anapaswa kutulia na kuzingatia matibabu anayopewa,” amesema.

The post JKT TANZANIA YAKARIBIA MALENGO YA MSIMU appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/8fs70ip
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post