HAKUNA MCHEZAJI MMOJA, USHINDI UNATOKA KWA UMOJA

KIUNGO wa Simba SC, Neo Maema, amesisitiza kuwa mafanikio ya timu hayategemei mchezaji mmoja pekee, bali mshikamano na umoja wa kikosi kizima.

Maema anaamini mshikamano huo ndio msingi wa safari ya Simba kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

“Umoja, morali na mshikamano wa timu ndiyo silaha muhimu zaidi. Hizi huchangia kuunda mazingira mazuri ya kushirikiana ndani na nje ya uwanja,” aamesema na ameongeza kuwa hali hiyo inachochea wachezaji kushirikiana kama familia moja.

Kiungo huyo amebainisha kuwa wachezaji wachache wanaweza kuamua matokeo ya mechi fulani, lakini timu yenye mshikamano na umoja ndiyo inayoweza kubeba mataji mwishoni mwa msimu.

Aneongeza kuwa mshikamano unazidi mbinu za kucheza pekee, na furaha yake kubwa inatokana na kuona wachezaji wakiwa na mshikamano huo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

“Najua inahitajika nini ili kushinda ligi. Mshikamano ni kiini cha mafanikio,” amesema Maema, amefafanua kuwa furaha iliyopo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo na namna wachezaji wanavyoshikamana ni jambo muhimu sana kwake.

Maema ameongeza kuwa timu ipo kwenye safari ndefu, hivyo wachezaji lazima waendelee kushikamana, mshikamano huo hauishii tu kwenye uwanja bali unapaswa kuonekana katika kila kipengele cha maisha ya timu.

Kiungo huyo ameahidi kwamba kikosi cha Simba kitaendelea kujipanga kwa kila mchezo, kuhakikisha kila mchezaji anatimiza majukumu yake kikamilifu na kusaidia timu kufanikisha malengo yake.

The post HAKUNA MCHEZAJI MMOJA, USHINDI UNATOKA KWA UMOJA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/XeKyMpF
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post