GUMBO AHAIDI, MORALI JUU KAMBINI YANGA

UONGOZI  Yanga SC umeweka wazi kuwa kikosi cha timu hiyo kipo katika hali nzuri ya kisaikolojia na kiufundi kuelekea mchezo muhimu wa kesho Jumamosi dhidi ya FAR Rabat, utakaochezwa nchini Morocco kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza akiwa Morocco, Mkuu wa Msafara wa Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Rogers Gumbo, amesema maandalizi ya mchezo huo yamefanyika kwa umakini mkubwa, huku viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wote wakiwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha timu inapata matokeo chanya.

Gumbo amesisitiza kuwa uongozi umeweka mazingira bora kwa kikosi kufanya kazi yake uwanjani, akieleza kuwa imani kubwa imewekwa kwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji waliopo kutokana na ubora na uzoefu walionao.

“Kama viongozi tumejipanga vizuri ili kufanikisha matokeo mazuri. Kwa aina ya benchi la ufundi na wachezaji tulionao, tunaamini watafanya vizuri na kupambana hadi dakika ya mwisho,” amesema Gumbo.

Ameongeza kuwa hali ya morali ndani ya kikosi ipo juu, jambo linaloipa timu hamasa kubwa kuelekea mchezo huo mgumu wa ugenini, huku akibainisha kuwa mshikamano uliopo kambini ni silaha muhimu kwa Yanga.

“Wachezaji na viongozi wote wana morali kubwa kwa ajili ya mchezo huu. Tunawaomba Watanzania waendelee kutuombea dua ili tuweze kupata matokeo mazuri,” ameongeza.

Yanga inahitaji kupata angalau sare au ushindi dhidi ya FAR Rabat ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, jambo linalofanya pambano hilo kuwa la kihistoria na lenye presha kubwa kwa pande zote mbili.

The post GUMBO AHAIDI, MORALI JUU KAMBINI YANGA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/xWb6d8q
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post