WINGA mpya wa Yanga, Buba Jammeh, ameweka wazi kuwa alitabiri kufunga katika mchezo wake wa kwanza baada ya kupata baraka kutoka kwa mama yake kabla ya mechi.
Buba alifunga mabao mawili yaliyoipa Yanga ushindi wa 2-0 dhidi ya Cosmopolitan ya First League katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa KMC, akianza kwa kishindo maisha yake ndani ya kikosi hicho.
Nyota huyo amesema kabla ya kwenda uwanjani alipiga simu nyumbani kwao na kumuomba mama yake amuombee ili aweze kufunga katika mechi yake ya kwanza.
Kwa mujibu wa Buba, mama yake alimpa maneno ya faraja na ushauri uliomtia nguvu, jambo ambalo lilimpa imani kubwa ya kufanya vizuri.
“Nilizungumza na mama yangu kabla ya mechi, nikamwambia aniombee. Nilikuwa na hisia kuwa nitafunga na kweli Mungu akajalia nikapata mabao mawili,” amesena Buba.
Hata hivyo, pamoja na mwanzo huo mzuri, winga huyo amekiri kuwa bado hajaonesha kiwango chake halisi kwa kuwa ndiyo kwanza ameanza kucheza katika ligi mpya.
Ameongeza kuwa kadri atakavyozidi kuzoea mfumo wa timu na ushindani wa ligi, ataendelea kuimarika zaidi mchezo huo ulikuwa maalum kwake kwa sababu ulikuwa wa kwanza akiwa na jezi ya Yanga, na anaamini mechi zijazo zitakuwa bora zaidi kwake binafsi na kwa timu kwa ujumla.
Buba pia hakusita kuwashukuru mashabiki wa Yanga kwa mapokezi makubwa waliyompa baada ya mchezo huo, hajawahi kushuhudia hali kama ile ambapo walimpongeza na hata kumpa zawadi ya fedha, jambo lililompa hamasa ya kupambana zaidi uwanjani.
Nyota huyo kutoka Gambia ni mmoja wa wachezaji wapya waliotua Jangwani kupitia dirisha dogo la usajili, na tayari ameanza kuonesha dalili za kuwa tegemeo jipya ndani ya kikosi cha Yanga.
The post BUBA AFICHUA SIRI YA MABAO MAWILI DHIDI YA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/k4iDPcL
via IFTTT
Post a Comment