KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amefichua jambo zito linaloihusu timu hiyo kuelekea michezo yake muhimu ya Ligi Kuu Bara, ikiwemo Kariakoo Derby, akisisitiza kuwa wachezaji wake wanafahamu thamani ya jezi wanayoivaa na wajibu mkubwa ulio mbele yao.
Barker amesema kikosi chake kipo tayari kupambana bila presha licha ya ushindani mkubwa uliopo katika mashindano yanayoendelea, ikiwemo Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB. kuwa uzoefu wa timu hiyo katika mazingira ya ushindani ni silaha muhimu katika kipindi hiki cha msimu.
Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amebainisha kuwa maandalizi ya timu yamekuwa mazuri, huku wachezaji wakionyesha morali ya juu kambini, jambo la msingi kwa sasa ni kuhakikisha kila mchezaji anatimiza wajibu wake ndani ya uwanja, hasa katika mechi zenye ushindani mkali.
“Kila mtu ndani ya timu anatakiwa kutimiza wajibu wake ndani ya uwanja hasa katika kipindi hiki ambacho kila pointi ina umuhimu mkubwa kwenye mbio za ubingwa,” amesema Barker, amesisitiza umakini na nidhamu ya hali ya juu.
Akizungumzia presha ya mashabiki na uzito wa mechi zijazo, Barker amesema Simba ni timu kubwa iliyozoea mazingira ya ushindani, hivyo wachezaji wake wanaelewa fika thamani ya jezi wanayoivaa na matarajio makubwa ya mashabiki wao.
Ameweka wazi kuwa benchi la ufundi limejipanga kimkakati kuhakikisha makosa yaliyopita hayajirudii kuelekea mechi zijazo, ikiwemo Kariakoo Derby ambayo ni muhimu katika mbio za kusaka alama za thamani.
Katika hatua nyingine, Barker amegusia uimara wa wapinzani wao, akieleza kuwa hakuna timu nyepesi katika ligi ya msimu huu. Hata hivyo, amesisitiza kuwa Simba haitabadilisha falsafa yake ya kucheza soka la kushambulia na kutafuta ushindi katika kila mchezo watakaocheza.
Simba ikiendelea na maandalizi ya mechi hizo ngumu, macho na masikio ya mashabiki wa wekundu wa Msimbazi yapo uwanjani kusubiri utekelezaji wa maneno ya kocha huyo, wakiamini timu yao itaonyesha makali yanayotarajiwa katika harakati za kusaka mafanikio msimu huu.
The post BARKER AWAONYA WACHEZAJI SIMBA, THAMANI YA JEZI appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/Poh5Nzk
via IFTTT
Post a Comment