Yanga yavunja mkataba na Andy Boyeli

 

Inaelezwa tayari Yanga imemalizana na mshambuliaji Andy Boyeli wakisitisha mkataba wake wa mkopo kutoka klabu ya Sekhukhune United ya Afrika Kusini.

Boyeli anarejea kwa waajiri wake hao baada ya kushindwa kutamba ndani ya kikosi cha Yanga.

Anaondoka Yanga akiwa amefunga mabao mawili katika ligi kuu ya NBC, mabao pekee aliyofunga katika mechi za mashindano.

Ni wazi haikuwa rahisi kwake kuvaa viatu vilivyowahi kuvaliwa na Mcongomani mwenzake Fiston Mayele aliyeacha alama Yanga kabla ya kutimkia Pyramids.

Mashabiki wa Yanga waliweka matarajio makubwa kwake lakini ni kama hakuweza kwendana na aina ya uchezaji wa Yanga.

Yanga tayari imeongeza mshambuliaji wa ndani Emmanuel Mwanengo katika dirisha hili dogo huku ikitarajiwa kushusha mshambuliaji mwingine wa kigeni kuchukua nafasi ya Boyeli.

Usikose kutazama mechi zote za Afcon, Mapinduzi cup, mechibzote za ulaya, ligi kuu Tanzania bara na nyingine nyingi LIVE kupitia Simu yako 

 download App hii mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA  AU HAPAAAA au HAPAA kumbuka app bado hayujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK hivo ikileta neno harmful usiogope ni kwasababu bado hatujaiweka playstore

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post