Kiungo mshambuliaji wa Vipers Fc Allan Okello anaushawishi uongozi wa timu hiyo umruhusu aweze kujiunga na Yanga katika dirisha hili la usajili, imefahamika.
Okello alikuwa Morocco na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda katika michuano ya Afcon 2025 ambao baada ya kurejea Uganda, wasimamizi wake wanampambania aweze kujiunga na Wananchi.
Vipers Fc wamegomea ofa ya awali iliyotolewa na Yanga wakitaka fedha zaidi. Ikumbukwe mchezaji huyo amebakisha miezi sita tu katika mkataba wake uliobaki na Vipers.
Yanga iko tayari kusubiri mkataba wake umalizike mwezi Juni ili wamsajili akiwa mchezaji huru.
Taarifa kutoka chanzo cha karibu na mchezaji huyo, imedokeza kuwa siku ya Jumatatu, Mawakala wa mchezaji huyo watafanya kikao na Rais wa klabu hiyo Lawrence Mulindwani ampe ruhusa mteja wao akasake changamoto mpya
Follow page yetu 👉🏻👉🏻 Bofya Hapa kufollow page yetu ili kuwa wakwanza kupata habari zote za michezo.
Usikose kutazama mechi zote za Afcon, Mapinduzi cup, mechibzote za ulaya, ligi kuu Tanzania bara na nyingine nyingi LIVE kupitia Simu yako
download App hii mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA AU HAPAAAA au HAPAA kumbuka app bado hayujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK hivo ikileta neno harmful usiogope ni kwasababu bado hatujaiweka playstore

Post a Comment