MUKWALA ATUA AL NASR

MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Uganda, Steven Mukwala ameondoka rasmi ndani ya  klabu hiyi baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Al Nasr ya Libya.

Mukwala amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hatua inayofungua ukurasa mpya katika taaluma yake ya soka.

Nyota huyo  ameondoka Simba baada ya kipindi alichopata uzoefu muhimu ndani ya kikosi hicho, akipambana kupata nafasi katika safu ya ushambuliaji iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Uamuzi wa kujiunga na Al Nasr unaelezwa kuwa ni mkakati wa mchezaji huyo kutafuta changamoto mpya nje ya Afrika Mashariki, hususan katika soka la Afrika Kaskazini ambalo linatajwa kuwa na ushindani na hadhi kubwa barani Afrika.

Kwa upande wa Simba SC, kuondoka kwa Mukwala ni sehemu ya mabadiliko ya kikosi yanayoendelea kufanywa na uongozi pamoja na benchi la ufundi, huku klabu ikilenga kuimarisha timu kwa ajili ya mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Mukwala alijiunga na Simba akitokea Ligi Kuu ya Uganda, katika muda aliokuwa Msimbazi aliweza kushiriki michezo mbalimbali ya ligi na michuano ya kimataifa, akionyesha uwezo wake wa kucheza kwa nguvu, kasi na kujituma kwa timu.

Sasa, macho ya mashabiki wa soka yataelekezwa Afrika Kaskazini kuona namna mshambuliaji huyo atakavyoitumikia Al Nasr, huku akitarajiwa kuitumia fursa hiyo kujiimarisha zaidi na kulipa imani ya klabu yake mpya.

The post MUKWALA ATUA AL NASR appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/caUg3oh
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post