LOEMBA NJIANI KUTUA SIMBA

BAADA ya klabu ya Simba kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Alain Anicet Oura, imeelezwa kuwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara wako hatua za mwisho kukamilisha dili la kiungo mwingine, Iñno Jospin Loemba, anayekipiga katika klabu ya Colombe Sportive du Lobo ya Cameroon.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Simba kuimarisha kikosi chake kuelekea mashindano muhimu yaliyo mbele yao, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya ndani.

Oura ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika baada ya kuwatumikia ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Stellenbosch SC ya Afrika Kusini, kabla ya kujiunga na Simba akitokea IF Gnistan ya Finland.

Kwa upande wa Loemba, dalili zote zinaonyesha kuwa usajili wake upo karibu kukamilika baada ya mchezaji huyo kuaga rasmi klabu yake ya Colombe Sportive du Lobo.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Loemba ametoa ujumbe wa shukrani na heshima kwa benchi la ufundi, wachezaji wenzake pamoja na mashabiki wa klabu hiyo.

“Hatua hii niliyopitia ndani ya klabu imekuwa uzoefu wa kipekee wa kibinadamu, kimichezo na kitaaluma wenye thamani kubwa, uliyoacha alama ya kudumu katika safari yangu na kuimarisha mafunzo niliyoyapata,” ameandika Loemba.

Ameongeza kwa kuwashukuru viongozi na mashabiki kwa imani waliyoonyesha kwake akisema, “Asanteni kwa imani mliyonipa, kujituma kwenu na nyakati zote tulizoshirikiana. Heshima na taadhima kwa Ndege wa Kusini, Colombe, daima juu zaidi.”

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Loemba yupo safarini kuelekea Tanzania na muda wowote anaweza kutua nchini kwa ajili ya kukamilisha makubaliano binafsi na klabu ya Simba, hatua itakayoongeza nguvu mpya ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

The post LOEMBA NJIANI KUTUA SIMBA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/5Y0zo73
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post