KISHINDO KIPYA UWANJANI NA MZIZE

BAADA ya kipindi kirefu cha kuwa nje ya uwanja, mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize, amerejea rasmi kuendelea na mazoezi ya ushindani uwanjani akiwa pamoja na wachezaji wenzake.

Mzize alianza kurejea taratibu kupitia mazoezi ya Gym, hatua iliyolenga kumjenga kimwili na kurejesha nguvu baada ya kupona jeraha lililomsumbua kwa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo alilazimika kukaa nje kwa kipindi kirefu akiuguza jeraha, baada ya kufanyiwa upasuaji uliohitaji muda wa kutosha wa mapumziko na uangalizi wa kitabibu.

Baada ya kukamilisha kwa mafanikio hatua za awali za mazoezi ya kurejesha utimamu, Mzize sasa amethibitishwa kuwa yupo fiti na tayari kwa mazoezi ya kawaida ya timu.

Kwa sasa, nyota huyo ameungana na wachezaji wenzake katika mazoezi yanayoendelea katika Uwanja wa KMC Complex, akionesha dalili nzuri za kurejea kwenye kiwango chake cha ushindani.

Kurejea kwa Mzize ni habari njema kwa benchi la ufundi la Yanga, ambalo linatarajia kupata chaguo zaidi katika safu ya ushambuliaji kuelekea michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano mengine.

The post KISHINDO KIPYA UWANJANI NA MZIZE appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/0CISgbN
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post