Nilipokutana naye mara ya kwanza, nilijua aliniangalia kwa upendo, lakini pia kwa masharti. Alikuwa bintiye chifu, mwenye heshima kubwa katika kijiji chake, na mara zote alikuwa akionekana kuguswa na matazamio ya familia yake.
Nilijua hatimaye nitapitia changamoto, kwani mimi sikua tajiri, na hofu ya kushindwa ilianza kupanda ndani yangu. Nilijaribu mara nyingi kuonyesha nia yangu. Nilimpeleka zawadi ndogo, nikamwonyesha heshima na dhati ya mapenzi yangu.
Lakini kila jaribio lilipoteza nguvu. Familia yake iliniona kama mtu wa chini, mtu ambaye hawezi kumlipa heshima ya cheo chake. Nilijikuta nikikosa tumaini, nikidhani kwamba kila kitu kimekoma kabla hata ya kuanza. Soma zaidi hapa

Post a Comment