USHINDANI WAZIDI KUCHEMKA, ABEL AJIPANGA SIMBA

Licha ya kuwepo kwa tetesi kwamba uongozi wa Simba  upo katika mchakato wa kutafuta kipa mwingine, hali hiyo haijamkatisha tamaa kipa namba tatu wa kikosi hicho, Abel Hussein, ambaye ameendelea kutumia muda wa mapumziko kujifua ili kujiweka tayari kwa changamoto zinazomkabili.

Abel amechukua hatua ya kuendelea na mazoezi binafsi kwa kushirikiana na timu ya vijana ya Simba, akilenga kuongeza kiwango chake cha utimamu wa mwili na ushindani, huku akisubiri kurejea rasmi kwa kikosi cha wakubwa.

Wakati huohuo, uongozi wa Simba unasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Daktari wa Taifa Stars kuhusu hali ya majeraha ya kipa Yakubu Seleman, ambaye alipata maumivu wakati akiwa kwenye mazoezi ya timu ya taifa.

Aidha, kipa namba moja wa Simba, Moussa Camara, anatarajiwa kurejea uwanjani mwishoni mwa mwezi Januari, hali inayoongeza ushindani katika nafasi ya ulinzi wa lango na kumlazimu Abel kuongeza juhudi zaidi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Kwa kutambua ushindani huo, Abel ameendelea kujinoa mapema kabla ya leo, siku ambayo kikosi cha Simba kinarejea rasmi mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza leo visiwani Zanzibar.

Kipa huyo namba tatu anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Simba katika mashindano hayo, akiwa na dhamira ya kuhakikisha analinda kwa uimara lango la timu pale atakapohitajika, sambamba na kuonesha uwezo wake kwa benchi la ufundi.

The post USHINDANI WAZIDI KUCHEMKA, ABEL AJIPANGA SIMBA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/mrfGUJx
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post