SIRI YAFICHUKA SIMBA KUKOSA MATOKEO, MAGORI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Crescentius Magori, ameweka wazi sababu kuu zinazosababisha timu hiyo kupata matokeo yasiyoridhisha katika baadhi ya mechi za hivi karibuni.

Magori amesema  majeraha ya wachezaji muhimu yamekuwa kikwazo kikubwa kwa kikosi hicho, hali inayomfanya kocha kushindwa kutumia nguvu kamili ya timu katika kila mchezo.

Amesisitiza kuwa hakuna kiongozi wa klabu anayeweza au anayeshawishi wachezaji kucheza chini ya kiwango chao kwa makusudi ili timu ipate matokeo mabovu, akieleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

Kwa mujibu wa Magori, changamoto ya majeraha imeikumba Simba katika kipindi ambacho timu ilikuwa katika mchakato wa mpito wa mabadiliko ya benchi la ufundi, jambo lililoathiri uimara wa kikosi.

Ameeleza kuwa kocha mmoja alianza kujenga timu kutoka chini, lakini akaondoka, akaja kocha mwingine naye akaondoka, huku baadhi ya wachezaji muhimu wakiwa nje ya uwanja kutokana na majeraha ya muda mrefu.

“Sio kweli kwamba viongozi wanawaambia wachezaji wacheze chini ya kiwango. Kifundi tumepata shida kwa sababu ya mabadiliko ya makocha na pia majeraha ya wachezaji wetu muhimu,” amesema Magori.

Amesema   hakuna mchezaji anayelipwa vizuri na klabu kwa lengo la kuipiga Simba, wala hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kumshawishi mchezaji acheze chini ya kiwango chake kwa maslahi binafsi.

The post SIRI YAFICHUKA SIMBA KUKOSA MATOKEO, MAGORI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/WoIOMkP
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post