KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mpya, Steve Barker kinatarajiwa kuondoka kesho Januari Mosi, 2026 kuelekea Visiwani Zanzibar.
Simba wanaelekea Visiwani humo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi, zinazokutanisha klabu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Safari hiyo ni sehemu ya maandalizi muhimu ya timu hiyo kuelekea nusu ya pili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara lakini pia kumpa muda Kocha Barker kuona madhaifu ya kikosi cha timu hiyo.
Mashindano ya Mapinduzi yanatajwa kuwa na ushindani mkubwa, hivyo Simba imechukua hatua ya mapema kupeleka kikosi chake kamili ili kuwapa nafasi wachezaji kupata mechi za ushindani na kuimarisha muunganiko wa timu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Simba itaanza kampeni yake katika mashindano hayo kwa kucheza mechi ya kwanza Januari 3 dhidi ya Muembe Makumbi City. Mchezo huo utapigwa saa mbili usiku, ukiwa ni moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka visiwani Zanzibar.
Kocha wa Barker anafanya wazi kwa lengo kubwa la timu si tu kushinda mechi, bali pia kuwapa nafasi wachezaji waliokuwa hawapati dakika nyingi za kucheza kuonyesha uwezo wao.
Michuano hiyo itatumika kama jukwaa la kupima mbinu mbalimbali za kiufundi, baadhi ya wachezaji muhimu wa Simba wanatarajiwa kuwa sehemu ya safari hiyo.
Huku wengine wakitarajiwa kutumia mashindano hayo kurejea kwenye kiwango chao bora baada ya kuandamwa na majeraha au kushuka kwa kiwango. Hali hiyo inaongeza ushindani wa nafasi ndani ya kikosi.
The post SIMBA SC KUELEKEA ZANZIBAR appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/uWnB6xy
via IFTTT
Post a Comment