SAFARI YA CLEMENT MZIZE YAANZA UPYA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize ameanza rasmi safari ya kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha ya mguu yaliyomuweka nje ya uwanja kwa kipindi fulani.

Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kumrejesha taratibu katika ushindani wa michezo.

Mzize kwa sasa anafanya mazoezi mepesi ya gym ikiwa ni sehemu ya mpango wa kurejesha nguvu na uimara wa mwili wake. Mazoezi hayo yanafanyika chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya wa klabu hiyo.

Nyota huyo ameonekana kuungana na wachezaji wenzake katika mazoezi ya gym, hali inayoashiria kuwa hali yake kiafya inaendelea kuimarika. Bado anaendelea kufuata programu maalum iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili yake.

Programu hiyo inalenga kumsaidia Mzize kurejea katika kiwango chake cha kawaida bila kuhatarisha afya yake, huku akipimwa hatua kwa hatua kabla ya kuanza mazoezi ya kawaida ya uwanjani.

Akizungumzia maendeleo hayo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema   Mzize ameanza mazoezi mepesi kwa lengo la kumrudisha katika hali bora ya ushindani.

Kamwe ameongeza  kuwa klabu inachukua tahadhari kubwa katika mchakato wa kurejesha mchezaji huyo ili kuepuka majeraha ya kujirudia, jambo ambalo linaweza kumrudisha nyuma zaidi.

Mashabiki wa Yanga sasa wana kila sababu ya kuwa na matumaini, wakisubiri kwa hamu siku ambayo  Mzize atarejea tena uwanjani na kuendelea kuisaidia timu yao katika mashindano mbalimbali.

The post SAFARI YA CLEMENT MZIZE YAANZA UPYA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/i1L4evH
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post