MLENGO AKIMBILIA JANGWANI, TRA UNITED BYE BYE

ALIYEKUWA mshambuliaji wa TRA United, Emmanuel Mwanengo maarufu kama “Mengo”, ameaga rasmi klabu hiyo baada ya kukamilisha makubaliano ya kujiunga na Yanga, hatua inayofungua ukurasa mpya katika taaluma yake ya soka.

Kuaga kwa Mengo kunakuja kufuatia taarifa za ndani zinazoeleza kuwa mshambuliaji huyo tayari amemalizana na Yanga,  anatarajiwa kutambulishwa muda wowote kuanzia sasa, ikiwa ni miongoni mwa usajili wa kwanza wa dirisha dogo la usajili.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Mengo aliwashukuru kwa dhati viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzake aliokuwa nao TRA United, akieleza kuwa imani na nafasi aliyopewa imekuwa chachu ya maendeleo yake binafsi.

“Shukrani zote ziende kwa watu wote walioniamini na kunipa nafasi ya kuwa sehemu ya timu hizi mbili bora, TRA United na Tabora United ya zamani,” aliandika Mengo katika ujumbe wake wa kuaga.

Mshambuliaji huyo aliendelea kuwapongeza makocha, viongozi na wafanyakazi wa timu kwa mchango wao katika safari yake ya soka, amesisitiza kuwa mwisho wa safari moja ni mwanzo wa safari nyingine, huku akituma salamu za upendo na shukrani kwa wote aliowahi kufanya kazi nao.

Kwa mujibu wa taarifa, Mengo anatarajiwa kuungana na kikosi cha Yanga kitakachosafiri kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambako atapata fursa ya kuanza safari yake mpya akiwa na mabingwa hao wa kihistoria.

The post MLENGO AKIMBILIA JANGWANI, TRA UNITED BYE BYE appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/f0EanqQ
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post